Rais Barrack Obama wa Marekani amekuwa miongoni mwa viongozi wakubwa wa dunia walioalikwa katika hafla ya kuapishwa kwa rais wa nne wa Kenya.
Mkuu wa Huduma za Jamii Francis Kimemia serikali imewaalika viongozi kama vile Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameroon na Mkuu wa Mataifa ya umoja wa Ulaya.
Pia wamealikwa marais wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) ikiwa ni pamoja na rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, rais Paul Kagame wa Rwanda na rais Pierre Nkurunziza wa Burundi.
Rais mpya wa Kenya anatarajiwa kuapishwa kuchukua madaraka hapo Machi 3 mwaka huu, ikiwa ni wiki tatu baada ya wakenya kufanya uchaguzi.