MPYA KUTOKA BEEF LA D'BANJ NA ALIYEKUWA MENEJA WAKE

Bankuli na D'Banj
Tiff ambalo lilikua linaendelea chinichini kati ya D Banj na aliyekuwa meneja wake, Abisagboola Oluseun John maarufu kama Bankuli limeibuka tena baada ya Bankuli mwenyewe kuibuka na kusema kuwa yeye mwenyewe ndiye aliyeamua kuacha kufanya kazi na D'Banj, na hajafukuzwa hata kidogo kama ambavyo story mtaani zinaeleza.
D'Banj na Bankuli kipindi bado wana-roll pamoja
Chanzo cha ugomvi wa wawili hawa kinatajwa kuwa ni Bankuli ambaye aliondoka kwenda kufanya kazi na Kanye West Ufaransa bila kumshirikisha D Banj, na kutokana na maelezo ya watu wa karibu, D Banj amekuwa ni mtu rahisi sana kuwaka pale anapogundua kuna mambo yanayoendeshwa chini chini na mtu wake wa karibu bila kumhusisha.

Kutonana na issue hii, Bankuli na D banj wamekuwa katika mlolongo wa ugomvi mpaka mwisho wa siku kila mmoja akachukua njia yake.

Bankuli Jay Z Kanye West
Meneja huyu ambaye pia na yeye ni msanii kwa sasa anaendesha kampuni yake ya BANKULI ENTERTAINMENT, na ndiye anayetajwa kuweza kumkutanisha D Banj na kaye West kwa mara ya kwanza huko Dubai...  mbali na kazi nyingi alizofanya yeye pia anasisika katika Chorus ya ngoma maarufu ya D Banj 'Oyato'.

Sikiliza Oyato hapa


Previous Post Next Post