MAMBO 7 MUHIMU KUTOKA KWENYE MAELEZO YA MTU PEKEE ALIEKUWEMO KTK GARI DEREVA ALILOPIGWA RISASI KINONDONI JUZI



Moja kati ya matukio makubwa ya kukumbukwa wiki hii siku ya jumatano march 20 2013 likiwa ni tukio la dereva wa gari dogo aina ya Corolla kupigwa risasi kwenye foleni Kinondoni na mtu aliekua kwenye pikipiki.
millardayo.com na Amplifaya ya Clouds Fm zilipata nafasi ya kuongea kwenye Exclusive interview na mtu pekee ambae alikua kwenye gari na marehemu kabla ya kupigwa risasi na kufariki papohapo wakitokea gereji.
Haya ni mambo 7  makuu aliyoyasema.
1. Kwenye eneo la Mkwajuni Kinondoni kulikua na lori aina ya fuso limesimama barabarani alafu wakati huo kulikua na mwarabu mmoja anaendesha pikipiki aliekua amewatangulia hawa jamaa, walikua kwenye upande wa kushoto wa barabara na mwarabu alikua upande wa kulia ambapo muda mfupi baadae mwarabu alijigonga kwenye ubavu wa fuso akarushwa upande wa kushoto alipokuepo Marehemu ambae aliweza kumkwepa na kuipeleka gari nje ya barabara kulikosababisha tairi kupasua.
2. Baada ya hapo walimfata mwarabu na kwenda kuongea nae, kwanza akawashukuru kwa kumkwepa kisha wakaanza kuongea nae kuhusu malipo, yani wa gari dogo walitaka walipwe tairi lao lililopasuka lakini ghafla bila kutarajia mwarabu alitoa nyaya za umeme zinazotoa shoti na akaanza kuwapiga shoti mwilini kwa makusudi hawa watu wawili waliokuwepo kwenye gari dogo.
3. Huyu shuhuda anasema huyu mwarabu anaitwa ‘Abuu’ na hilo jina lilifahamika baada ya watu kadhaa kujitokeza kwenye eneo la ajali na kumsisitiza asifanye fujo wala kuwapiga wenye gari manake wameokoa maisha yake kwa kumkwepa.
4. Baada ya ubishi huku dereva akiuliza sababu zipi zilizofanya apigwe shoti yeye na mwenzake, mwarabu huyu alichukua bastola yake iliyokua chini na kumfyetulia risasi dereva na kufariki palepale kwenye tukio na mwarabu kukimbia na pikipiki yake.
5. Marehemu hafahamiani na mwarabu huyu hata kidogo ambapo pia shuhuda anasema  mazungumzo ya mwisho ya marehemu ni kuhusu mpango wa kuoa July au August mwaka huu.
6. Mtuhumiwa huyu ambae inadaiwa alikua amenyoa panki alionekana na chupa kubwa ya kinywaji maarufu chenye kilevi ambacho kinatengenezwa nje ya Tanzania ambacho husifika na wengi kwa ukali wake wa kulewesha muda mfupi tu baada ya kunywa.
7. Marehemu aliezikwa march 21 2013 saa kumi jioni kwenye makaburi ya kinondoni alikua ameajiriwa kama msaidizi nyumbani ambapo miongoni mwa majukumu yake ni kutumwa sehemu mbalimbali kufanya shughuli za mwajiri wake.
8. Polisi wameahidi kuzungumza leo.
Previous Post Next Post