KINANA AZUNGUMZA NA WAZIRI ANAYESHUGHULIKIA MASUALA YA CPC CHINA, ATEMBELEA CHINALCO


1. KINANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Waziri anayeshughulikia mambo ya chama katika Chama Cha Kikomunisti cha China, Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye Ofisi za CPC, mjini Beijing, China na kuwa na mazungumzo naye. Nyuma ya Kinana ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai. 
2. KINANA AKIZUNGUMZA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na waziri anayeshughulikia masuala ya chama wa Chama cha Kikomnisti cha China, Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye Ofisi za CPC, mjini Beijing, China. 3. KINANA AKIKAGUA
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akitazama baadhi ya malighafi, alipotembelea kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO), alipotembelea kiwanda hicho mjini Beijing,  Machi 20, 2013. Wapili kulia ni Rais wa Kampuni hiyo Xiong Weiping (Picha na Bashir Nkoromo). 4. KINANA AKIWEKA MAONI KITABUNI
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitia saini kweneye kitabu maalum cha wageni, katika kampuni ya Aluminum ya China ((CHINALCO). Kushoto ni Rais wa Kampuni hiyo, Xiong Weiping na wapili kushoto ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Khamis Suleiman Dadi. (Picha na Bashir Nkoromo). 5. KINANA NA UJUMBE WAKE KIWANDA CHA ALUMINIUM
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na uongozi wa CHINALCO, Kinana na ujumbe huo walipotembelea kampuni hiyo wakiwa katika ziara ya mafunzo Beijing, China. 6. KINANA AKITOA KINYAGO
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa zwadi ya kinyagoo cha Kimakonde cha aina ya ‘Ujamaa’, Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo nchini China. (Picha na Bashir Nkoromo). 7. KINANA AKIKABIDHIWA ZAWADI ALUMINIUM
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipewa zwadi ya pambo la Kichina, na  Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, Kinana alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo nchini China. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. (Picha na Bashir Nkoromo).
Previous Post Next Post

Popular Items