GFC YAASISITIZA KATIBA MPYA KUTOPUUZA UTU WA MWANAMKE NA MTOTO


1Mwenyekiti wa muungano wa jinsia na katiba(GFC) Magdalena Rwebangira (kulia) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa kutathmini marekebisho na mtazamo wa rasimu ya katiba mpya uliofanyika katika hotel ya Bruel Pearl, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake (Tawla), Aisha Bade

2Wanaharakati na Madiwani mbalimbali wakifuatilia ajenda zinazowasilishwa kupitia muungano wa jinsia na katiba(GFC) juu ya mtazamo na maoni ya kijinsia yanayopendekezwa kuwasilisha kwenye katiba mpya, ndani ya hotel ya Bruel Pearl Ubungo Dar es Salaam
3Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake (Tawla), Aisha Bade akisisitiza jambo katika mkutano wa kutathmini marekebisho na mtazamo wa rasimu ya katiba mpya uliofanyika katika hotel ya Bruel Pearl, jijini Dar es Salaam na kujumuisha wanaharakati na madiwani kutoka manispaa za jiji la Dar es Salaam. 4Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake (Tawla), Tike Mwambimbipile akifuatilia mchakato wa marekebisho na upitiaji maoni ya rasimu ya katiba mpya katika mkutano uliojumuisha wadau mbalimbali wa jinsia ndani ya hotel ya Bruel Pearl, Ubungo Dar es Salaam 5Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake (Tawla), Aisha Bade,aliyesimama akishauriana jambo na Afisa Mradi Kitengo cha Ardhi Tawla, Latifa Mwabondo,  wakati wa mkutano wa kutathmini marekebisho na mtazamo wa rasimu ya katiba mpya uliofanyika katika hotel ya Bruel Pearl, jijini Dar es Salaam.   
6Mwanasiasa mkongwe , Getrude Mongela, akichangia mada kwenye mkutano huo.
7
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Uenezi wa Tawla, Naseku Kisambu (wa kwanza kulia) akipitia moja ya vipeperushi vilivyoainisha maoni kuelekea uandikaji rasimu ya katiba mpya katika mkutano uliojumuisha wadau mbalimbali wa jinsia jijini Dar es Salaam
 HABARI PICHA NA JR BOTEA WA 4BROTHERS IN NEWS
………………………
……………………………………………………
WANAHARAKATI na wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya jinsia katika mchakato wa kuandika katiba mpya nchini wamependekeza katiba mpya itambue na ijumuishe haki zinazojulikana kama haki za kizazi cha kwanza, cha-pili na cha-tatu, na zijumuishwe kama haki za msingi kwani zote ni muhimu katika kulinda utu wa mwanamke na mtoto.
Akizungumza Dar es Salaam leo katika mkutano wa kutathmini, kufahamiana na kujua yanayojiri katika mchakato wa kurekebisha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kuandika Katiba Mpya, Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake (Tawla), Aisha Bade, amesema pamoja na mambo mengine, haki hizo ni za kiraia, kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
 “Bila ya haki hizo kutambuliwa na kulindwa na katiba, maisha ya wanyonge tunayoyaimba kila kila siku hayataweza kuinuliwa…haki kama za ndoa, kumiliki mali, uraia na nyinginezo ni muhimu kuzingatiwa katika mchakato wa rasimu ya katiba mpya,” amesema Bade
Aidha ameshauri katiba ijayo iwe na kipengele kinachohusu haki sawa ya kumiliki ardhi kwa wanawake, watoto na makundi mengine maalum, ikiwemo umilikishwaji wa rasilimali zote za taifa kwa wananchi.
 Naye Mwenyekiti wa Muungano wa Jinsia na Katiba (GFC), Magdalena Rwebangira, amesema lengo hasa la wao kukutana ni kufanya tathmini sanjari na kuangalia namna nzuri watakavyoteua wawaakilishi watakaosimamia na kuwasilisha maoni na mitazamo yao juu ya katiba mpya kwenye mabaraza ya kata ya wilaya.
 “Ndio maana tumejumuika pamoja na madiwani ili wafahamu tunachokijadili kwa sababu wao wataingia kama wajumbe kwenye mabaraza hayo, ambapo pamoja na mambo mengine maoni juu ya mchakato wa katiba mpya tumependekeza yawe katika mtazamo wa kijinsia,” amesema Rwebangira, na kuongeza:
 “Hili ni tukio la kihistoria, na ni tukio ambalo kama litafanyika kwa viwango na matakwa ya watanzania hakika litaliweka Taifa katika taswira chanya kimataifa.”
 Hii ni mara ya nne mkutano huo kufanyika mkoa wa Dar es Salaam, maeneo mengine ulipofanyika mkutano huo ni pamoja na Zanzibar, Mwanza, Lindi na Kilimanjaro
Previous Post Next Post