KELLY AMCHARUKIA JUSTIN BIEBER





Kutokana na kitendo cha muimbaji Justin Bieber kuchelewa kwa muda wa masaa mawili katika onyesho lake lililofanyika  wiki  hii muimbaji na mtunzi wa muziki Kelly Jones ambwatukia Justin Bieber akidai kuwa anastahiri kuchukuliwa adhabu kali

Kuchelewa huko kulisababishwa na muimbaji huyo kuwasili kwenye uwanja wa Londonis O2 Arena akiwa amechelewa na kuwafanya baadhi ya mashabiki kuondoka bila kushuhudia shoo yake

Pamoja na hayo msanii huyo kila akitakiwa kutoa maelezo ya sababu inayomsababisha kuchelewa hudai kuwa ni sababu zinazosababisha kuchelewa kwake ni za kiufundi huku muimbaji Kelly akiongea na gazeti la 'The Sun' kuwa muimbaji huyo mwenzake anatakiwa kupewa adhabu kwa kitendo anachokifanya cha kuchelewa kwenye shoo zake mara kwa mara
Previous Post Next Post