HUU NDIO UKWELI KUHUSU UTAJIRI WA KIM KARDASHIAN!


Baada ya tukio la kuibiwa kwa taarifa za siri za mastaa mbalimbali hivi juzi, sasa story mtaani zimemuelemea mwanadada Kim Kardashian kutokana na siri juu ya utajiri wake kuonyesha picha ya tofauti na yeye alivyo.
Kim Kardashian
Imefahamika kuwa, licha ya umaarufu na dili zote ambazo Kim anazipiga, akaunti yake ya benki ina dola elfu 10 tu za kimarekani. (Hii ni sawa na shilingi milioni 16 na laki 2 tu za kitanzania).

Japo pesa hii inaweza kuonekana kama ni nyingi, lakini taarifa hizi zimeweka wazi pia kuwa, Mwanadada huyu ana deni la dola Milioni n5.6 ambazo amewekea dhamana Jumba lake lililokuwa huko LOS ANGELES ambapo kila mwezi anatakiwa kulipa dola elfu 26 sawa na shilingi milioni 42 na laki 2.
Nyumba ya Kim
Kim Kardashian
Juu ya hili pia Gari analotumia mwanadada huyu kwa sasa, G63 Mercedes SUV linatakiwa kulipiwa dola elfu 2, sawa na shilingi milioni 3 na laki 2 kila mwezi.
Kim Kardashian
Kwa kulinganisha mambo yote haya na vitu vingine vidogovidogo Hali ya uchumi ya mwanadada huyu imeonekana kuwa ni ya kusuasua na kuupa nguvu ule usemi wa'kidhungu' wa DONT JUDGE A BOOK BY ITS COVER.
Previous Post Next Post