HIVI NDIVYO VIMBWANGA VYA LADY GAGA BAADA YA OPARESHENI

Lady Gaga

Mara baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye moja ya hips zake, Lady Gaga ametengenezewa kiti maalum cha kutumia hadi pale atakapokuwa fiti kutembea mwenyewe.

Kiti hiki ni cha dhahabu safi kwa asilimia 99, yaani '24 carat Gold' na ni kazi safi ya ufundi ya sonara mtaalam wa mitindo anayefahamika Ken Borochov ambaye alitumia muda wa wiki moja kukamilisha kazi ya kutengeneza kiti hiki.





Hatua hii ni kielelezo tosha kuwa Gaga ni staa pekee ambaye ana mapenzi ya kipekee kwa mitindo ambayo siku zote huwa na mtazamo wa kipekee sana.
Previous Post Next Post