POLISI Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, linawashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za ujambazi walioufanya katika nyumba ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba Februari 3 mwaka huu. Ujambazi huo ulifanywa wakati naibu waziri huyo akiwa safarini jimboni kwake Bumbuli huku nyumbani hapo ikiwepo familia yake ambapo mlinzi alifungwa kamba na kuzibwa mdomo na majamazi hao.
Katika tukio hilo majambazi hao hawakukamilisha azima yao kwa kuwa mke wa naibu waziri huyo alibonyeza kengele ya tahadhari mapema ambayo ilipiga kelele zilizowaogopesha majambazi hao ambao walikimbia ili kujiokoa na kukamatwa. Baada ya tukio hilo,Kamanda wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyela aliahidi kuwasaka na kuwakamata watu waliohusika.
Source: Mwananchi