TANZANIA YASHIRIKI UTALII HISPANIA


1Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)Devota Mdachi  kushoto na maafisa wengine wakiwa katika maonyesho ya Utalii ya FITUR ambayo ni ya tatu kwa Duniani yaliyofanyika kuanzia Januari 30 mpaka Februari 3 mwaka huu nchini Madrid nchini Hispania  na kushirkisha Bodi ya Utalii (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa ya Ngorongoro (NCAA) na makampuni zaidi ya sita ya utalii kutoka nchini Tanzania  katikati ni  Esther Solomon (Senior Tourist Information Officer,(TTB) , Israel Naman ({Principal Conservation Officer, (NCAA) na Maria Kirombo (Park Warden, Arusha National Park).

2
Devota Mdach kushoto, Maria Kirombo and Esther Solomon wakiwa katika banda la Tanzania nchini Hispania kwenye maonyesho ya utalii ya FITUR.
3
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Youssou Ndour Waziri wa Utalii na Utamaduni nchini Senegal  ambaye pia ni mwanamuziki maarufu duniani wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho hayo , Youssou Ndour amewahi kufanya ziara ya kimuziki mara tatu nchini Tanzania kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na Utamaduni nchini mwake.
Previous Post Next Post