POLISI IRINGA YAIBAMIZA MKAMBA RANGERS


100 1149 2fd0b
Na: Denis Mlowe, Iringa
TIMU ya Polisi Iringa juzi iliweza kuibuka na ushindi baada ya kuifunga Mkamba Rangers ya Morogoro 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza uliochezwa uwanja wa wa Samora mkoani Iringa. Polisi ambayo ipo kundi A imefikisha pointi 14 na kukamata nafasi ya pili katika kundi ambalo linaongozwa na Mbeya City. Mabao ya...
Polisi Iringa yalifungwa na Dimoso Balika dakika ya 1, Hamad Kambangwa dakika ya 22 na Kassimu Kilungo kunako dakika ya 42 na lile la kufutia machozi kwa upande wa Mkamba Rangers lilifungwa na Kamugisha Edson katika dakika ya 87.
Timu ya Polisi Iringa ikiwa chini ya kocha Khalfan Ngasa wakiwa na jezi nyekundu iliweza kutawala mchezo katika vipindi vyote kwa kuweza kuwakimbiza watakavyo timu ya Mkamba Rangers iliyo chini ya kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga Keneth Mkapa wakiwa na jezi za njano na kufanya upinzani wa Simba na Yanga kuonekana kwa timu zote kwani Ngasa ambaye ni baba wa kiungo mshambuliaji wa Simba Mrisho Ngasa alikuwa mchezaji wa Simba na Keneth Mkapa alikuwa wa yanga hivyo mashabiki kuweza kufananisha kama Simba na Yanga.
Timu ya Mkamba iliweza fanya mabadiliko ambayo hayakuweza kuleta mafanikio kwa kuwatoa Isack Amoni na nafasi yake kuchukuliwa Seleman Salum na Hamis Rajabu alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Novatus Mapoyola. Mchezo huo iliochezeshwa vema na mwamuzi Mary Kapinga kutoka Songea ulimalizika kwa kutokuwa na kadi yoyote na wadau mbalimbali kumsifia mwamuzi huyo kwa kuchezesha kwa haki.
Makocha wa timu zote waliweza kusifu uamuzi mzuri wa refa na kila mmoja kulalamika kuhusiana na maandalizi hafifu wa timu zao. Mechi itakayofata ni Polisi Iringa kukutana na vinara wa kundi A Mbeya City wakati Mkamba watakutana na Burkina Faso.

Previous Post Next Post

Popular Items

Wajue Wanamuziki 10 Matajir Africa

AS CANNES YAMWAGIA SIFA KAPOMBE