Lino Oviedo enzi za uhai wake.
Mgombea wa urais nchini Paraguay, Lino Oviedo amefariki dunia katika ajali ya helikopta.
Oviedo, mwanajeshi mstaafu aliyekuwa na cheo cha Jenerali, alikuwa akisafiri kuelekea kwenye kampeni kaskazini mwa nchi hiyo, akiwa pamoja na mlinzi wake.
Rubani wa helikopta hiyo alitoa taarifa ya hali mbaya ya hewa kabla ajali hiyo haijatokea na kusababisha vifo vya watu wote watatu waliokuwemo ndani.
Oviedo alisaidia kuongoza mapinduzi miaka 24 iliyopita na kumuondoa madarakani dikteta Alfredo Stroessner ambaye alikuwa madarakani tangu mwaka 1954.
eneo la ajali.
Wafuasi wa Lino wakimlilia kwa Uchungu.
Mwili wa aliyekuwa mgombea wa Urais nchini Paraguay Lino Oviedo, ukipelekwa kuhifadhiwa.