![]() |
| Balozi wa Finland nchini Sinikka Antila |
BALOZI wa Finland nchini, Sinikka Antila, amewetaka viongozi wa Tanzania kusimamia vizuri matumizi ya maliasili kutokana na maliasili hizo, kuwa ndiyo ufunguo wa ukuaji wa maendeleo ya nchi.
Antila alitoa kauli hiyo, jijini Dar es Salaam jana, wakati wa mkutano uliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi, kwa ajili ya uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi wa Kijani, uliowakutanisha viongozi wa taasisi mbalimbali kujadili ushirikishwaji wa jamii katika kusimamia ukuaji wa uchumi.
Alisema katika nchi hiyo ya Finland maliasili, hususan viwanda vya mbao, vimetoa mchango mkubwa katika kuendeleza uchumi na kupunguza umasikini.
“Kwa ujumla vitu hivi viwili vinakwenda pamoja, mkono kwa mkono, uchumi unapokuwa umasikini unapungua zaidi hasa kama sera za kupunguza tofauti katika maisha zipo”alisema Antila.
Antila alisema hali hiyo inatarajiwa kuonekana Tanzania kutokana na taasisi hiyo ya Jukwaa la Uchumi wa Kijani kuweka umuhimu mkubwa kwenye mazingira na matumizi endelevu.
Awali akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais, waziri wa ofisi ya Mazingira, Terezya Huvisa, alisema mkutano huo unajadili mambo muhimu ya mazingira na maendeleo, anatarajia washiriki watatoka na majawabu yatakayoisaidia jamii.
Alisema anatambua kuwa Jukwaa hilo linapanga mikakati mipya ambayo itasaidia kutengeneza nafasi za ajira zitakazotokana na usimamiaji bora wa maliasili.
“Ni lazima tuondokane na mawazo kuwa kuwa kila kitu tumekirithi kutoka kwa wazazi wetu, baadala yake ni lazima tuzitunze maliasili hizi kwa ajili ya vizazi vyetu vinavyokuja”alisema Dk Bilali.
Alisema viongozi wote wanapaswa kujakuikabidhi nchi hii katika kizazi kijacho ikiwa na mazingira bora kulikoni inavyoonekana sasaa.
Naye waziri wa ofisi ya makamu wa rais (Mazingira) Huvisa, alisema kama nchi za Afrika hazitaunganisha nguvukatika kusimamia utunzaji wa mazingira kuna hatari nchi hizo kjikuta zikizorota kiuchumi.
Aidha, Tanzania itakuwa mwenyeji wa siku ya mazingira Barani Afrika itakayoadhimishwa Machi 3 mwaka huu, ambako maadhimisho hayo yatafanyika mkoani Arusha.
Tags:
Social
