MH.EDWARD LOWASSA AWAANGUKIA VIONGOZI WA DINI


kkkt 73eb2
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa,akisalimiana na na mchungaji  Trafaina Aseri Nkya ambaye pia ni msmaidizi wa askofu mteule wa Dayosisi ya KusiniMmashariki mwa Ziwa Victoria walipofika nyumbani kwa Mh Lowassa eneo la Ngarashi Monduli, kumshukuru kwa harambee ya ujenzi wa kanisa lao aliyoiendesha January mwaka jana na kupatikana kiasi cha shilingi millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi

kkkt1 826ca
Akizungumza na ujumbewa kamati ya ujenzi wa kanisa hilo

kkkt2 0bdad
Hapa Akiwasindikiza
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa, amewataka vingozi wa dini nchini, kusaidia kurejesha hali ya amani kati ya wasilam na wakiristo ambayo inaonekana inaanza kupotea.
Akizungumza nyumbani kwake Monduli, wakati alipokuwa akipokea ujumbe  kutoka kanisa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Lowassa amesema vurugu na mauaji yaliyotokea huko Buserere, yanasikitisha sana na kuongeza kuwa ni dalili mbaya  ya kutoweka kwa amani ya Tanzania.
``Rais ameelezea masikitiko yake, kwakweli inasikitisha sana, mimi nawaomba viongozi wa dini na madhehubu yote wasimamie kuzuia mambo haya, nawaomba watanzania wenzangu tusali kwa imani zetu kuomba amani yetu isipotee`` alisema Lowassa kwa masikitikiko makubwa.
Katika fujo hizo za Buserere,mchungaji  mmoja aliuawa baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya waislam na wakristo.Chanzo cha mapigano hayo kilikuwa ni wakristo kuamua kuchinja ngombe na kuuza kwenye bucha lao, hatua iliyopingwa na wananchi wa dini ya kiislam kwenye eneo hilo.
Ujumbe uliyofika nyumbani kwa Mh Lowassa uliongozwa na msaidizi wa askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya kusini mashariki mwa ziwa victoria, ulifika kumshukuru kutokana na kusimamia na kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa kuu la Shinyanga January mwaka jana ambapo zaidi ya shillingi millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana.
Previous Post Next Post

Popular Items

Music: Nikki Mbishi - Utamwambia nini

Magazetini Leo Ijumaa ya Tarehe 20/9/2013