CCM WAPATA SALAMU KUTOKA UINGEREZA




Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi TAWI la Uingereza, wanapenda kuungana na
Wanachama wenzao Tanzania na popote pale walipo duniani katika kusherehekea
miaka 36 ya kuzaliwa na
kushika hatamu kwa Chama Chetu cha Mapinduzi.
Kwa furaha tumekuwa pamoja kimawazo tukifuatilia kwa ukaribu maadhimisho
ya kitaifa ya sherehe za Miaka 36 yaliyofanyika kwenye Mkoa wa Kigoma na
Kufikia kilele chake Leo Jumanne. Ni dhahiri na tumeshuhudia maelfu ya
Wana-Kigoma na Watanzania wote kwa ujumla walijitokeza kwa wingi katika
kuadhimisha siku hii, yote haya yanaonyesha mapenzi ya Watanzania kwa
Chama Cha Mapinduzi.

Wana CCM UK tunatambua ya kuwa Chama Cha Mapinduzi tumefika hapa tulipo
kutokana na jitihada za kimapinduzi za waasisi wetu na waazilishi wa vyama
vya TANU na ASP , chini ya Uongozi wa Baba Wa Taifa - Marehemu Mwalimu
Julius K Nyerere na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume . CCM hii ya leo
imesimama imara kama matunda ya hekima na busara za wazee wetu na kuona
mbali kwa kuvunja vyama vya TANU na ASP kwa taadhima kubwa na kuunda Chama
kimoja madhubuti cha Siasa nchini Tanzania . Miaka 36 baadae CCM imeendelea
kutunza umoja, amani na upendo ,kwa kurithi yale waliyoaacha wazee wetu.
Tunawashukuru sana na kuwaombea Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi.
Wana CCM-UK , Tunapenda kutoa pongezi na shukrani zetu kwa Viongozi wetu
wote wa CCM waliopita kwa kusimamia na kuingoza nchi chini ya CCM na
kuweza kudumisha amani , upendo na umoja wa ndani na nje ya Tanzania.
Tanzania ,chini ya Chama Cha Mapinduzi ilikuwa katika mstari wa mbele
katika kuikomboa Afrika , na kushirikiana na wenzetu wa nchi nyingine za
Afrika kisiasa na kijamii, hususani katika Umoja wetu wa nchi za Afrika
Mashariki.
Wana CCM-UK ,Tunapenda tutoa pongezi za dhati na za pekee kwa Uongozi wa
sasa wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wetu Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete , katika kuiongoza nchi kwa upendo, amani na utulivu. Pongezi zetu
zaidi kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na
viongozi wake, katika kutekeleza sera za CCM kupitia Ilani za Uchaguzi za
Mwaka 2005 na 2010. Nchi yetu imepiga hatua kubwa sana kimaendelea chini
ya CCM na Tunatambua na kupongeza maendeleo nchini Tanzania yaliyotokana na
Sera za CCM.
Ni jamabo la kujivunia sana kwa Wana- CCM hususani katika kipindi hiki
kigumu chenye changamoto ambazo zimeikumba dunia nzima katika hali ya
kiuchumi na mabadiliko ya kisiasa,kuona kwamba CCM imeweza kusimama
madhubuti na imara na kuendelea kuongoza Nchi kwa amani. Licha ya
changamoto zinazojitokeza mara nyingine, kubwa na la msingi tunawapongeza
sana Viongozi wetu na wananchi wa Tanzania kwa kuendelea kusimamamia na
kudumisha hali ya utulivu, amani na upendo miongoni mwa Watanzania wote
ndani na nje ya nchi.
Wana –CCM UK tunajivunia hali ya CCM kushirikiana pamoja na Vyama vingine
vya siasa ndani ya Tanzania kwa nia na lengo la kuiletea maendeleo nchi
yetu . Hii inadhihirisha ukomavu wa Demokrasia wa hali ya juu na CCM
imekuwa ni mfano wa kuigwa na vyama vingi vya siasa barani Afrika , na
vilevile vyama vya siasa nchini Tanzania.
Wana CCM –UK na Dispora kwa ujumla,tunaendelea kushukuru kwa busara na
hekima za mwenyekiti wetu wa CCM Dr.Jakaya M Kikwete, kwa kuwezesha matawi
ya chama tawala nje ya nchi kufanya kazi, hili limewapa nafasi wapenzi wa
Chama Cha Mapinduzi na Watanzania waishio nje ya nchi kuweza kupata nafasi
ya kuchangia maendeleo na yale mazuri tuliyojifunza nje katika nyanja za
kisiasa na kiuchumi na kurudisha nyumbani kwa manufaa ya nchi yetu kwa
ujumla.
Kwa Watanzania wenzetu , wana ccm wenzetu ,tunawashukuru wote na tunaomba
tuendelee kudumisha amani ,upendo,na utulivu wetu ambao umekuwa ni ngao na
ni sifa ya Tanzania popote uendapo duniani. Bila ya Chama Cha Mapinduzi ,
Tanzania ingekuwa wapi ?
Happy Birthday Chama Cha Mapinduzi
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania.
UMOJA NI USHINDI.
Imetolewa na Idara ya Itikadi, Siasa na Uenezi
CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA UINGEREZA.
Previous Post Next Post