BULEMBO ATEMBELEA RUFIJI


 BULEMBO akikagua gati la kuegemeshea meli linaloendelea kujengwa katika wilaya ya mafia. Gati hilo ambalo ni muhimu sana kwa wananchi wa wilaya hiyo linatarajiwa kumalizika mwezi wa tatu mwaka huu. Wengine katika picha ni viongozi wa CCM.

  MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi tanzania, Abdallah Bulembo akizungumza na Mkuu wa kituo cha polisi cha wilaya ya Mafia kuhusu malalamiko ya askari wa usalama barabarani wa kituo chake, aliyetajwa kwa jina moja la Luka kwamba amekuwa akijihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa akimtaka afanye utaratibu wa kumuhamisha katika kituo hicho ili kurudisha heshima ya jeshi hilo kwa wananchi wa wilaya hiyo. Mkuu huyo wa kituo alimuahidi Bulembo kulifanyia kazi suala hilo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mafia Sauda Mtondoo.Picha na Mpiga Picha Maalum
Previous Post Next Post

Popular Items