DKT.BILAL ZIARANI MAREKANI


005 2a8ee
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo na Seneta, James Inhofe wa Jimbo la Oklahoma, wakati alipomtembelea Ofisini kwake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Seneta huyo jana Feb 6, 2013. Makamu wa Rais yupo nchini Marekani katika jiji la Washngton Dc kwa ziara ya siku nne. Picha na OMR

006 26dca
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi Johnnie Carson, wakati makamu alipofika Ofisini kwa Balozi huyo kwa mazungumzo leo, Feb 7, 2013. Balozi Carson ni msaidizi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika. Picha na OMR
007 8d2ce
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Mfuko wa MCC, Daniel Yohannes, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kuhusu kuendelea kwa mradi wa MCC ii, nchini Tanznia. Mazungumzo hayo yalifanyika jana Feb 6, 2013 katika Hoteli ya Omni iliyopo Washngton Dc Marekani, ambapo Makamu yupo nchini humo kwa ziara ya siku nne. Picha na OMR
Previous Post Next Post