WABUNGE wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii wamekanusha uvumi ulioenea Mwanza kuwa wamepewa fedha na uongozi wa Halmshauri ya Jiji la Mwanza, kuzima sakata la kutapeli Sh1.6 bilioni za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wabunge hao walisema taarifa zinazoenezwa siyo za kweli na kwamba, zina lengo la kuwavunja nguvu lakini msimamo wao upo thabiti .
Walisema watasimamia haki kuhakikisha NSSF inapatiwa viwanja au inalipwa fedha zake na fidia.
Walisema watasimamia haki kuhakikisha NSSF inapatiwa viwanja au inalipwa fedha zake na fidia.
Taarifa zilizoenea zinadai kuwa, uongozi wa Jiji la Mwanza uliwasiliana kwa faragha na baadhi ya wabunge hao na kuwapatia Sh12 milioni kuzima suala hilo kabla ya kuwasilishwa kwa spika.
Taarifa hizo zinadai baadhi ya wabunge hao walipokea fedha hizo kutoka kwa uongozi wa halmashauri kwenye hoteli moja maarufu mjini hapa, jambo ambalo limekanushwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Willison Kabwe.
Mbunge wa Mchinga, Saidi Mtanda (CCM) alikanusha uvumi huo na kueleza kuwa jambo hilo haliwezi kuzimwa na wabunge, hivyo kushangazwa na uvumi huo.
Mtanda alisema ingawa siyo jambo rahisi kuwazuia watu kueleza hisia zao, lakini kwa mazingira yaliyopo na msimamo wa kamati yao haliwezekani na kubainisha kwamba, wajumbe ni wengi.
Mtanda alisema ingawa siyo jambo rahisi kuwazuia watu kueleza hisia zao, lakini kwa mazingira yaliyopo na msimamo wa kamati yao haliwezekani na kubainisha kwamba, wajumbe ni wengi.
“Kamati ilishatoa uamuzi wake na pande zote mbili zilihusishwa, sasa kama kuna watu wametoa fedha kutafuta kupendelewa huko ni kupoteza fedha zao, kamati yetu inao wabunge zaidi ya wawili sasa utampa nani?” alihoji Mtanda na kuongeza:
“Lakini kama kweli wametoa fedha ngoja tusubiri uamuzi wa mwisho wa kamati na taarifa ambayo itakabidhiwa bungeni.”
“Lakini kama kweli wametoa fedha ngoja tusubiri uamuzi wa mwisho wa kamati na taarifa ambayo itakabidhiwa bungeni.”
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alieleza kusikitishwa na taarifa za baadhi yao kudaiwa kuhongwa ili kuzima suala hilo na kubainisha kuwa, iwapo kuna mbunge atakuwa amekubali kuhongwa atakuwa ameuza utu wake.
“Tupo wengi, sasa siwezi kujua rohoni mwa wenzangu, lakini kama kuna mbunge ameshiriki hilo kama linavyoelezwa basi atakuwa amenisikitisha sana,” alisema Lusinde.
Kwa upande wake, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Juma Nkamia alisema binafsi haitambui hoteli ambayo imetajwa kukutana na viongozi wa halmashauri ili kuwapa fedha hizo.
Kwa upande wake, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Juma Nkamia alisema binafsi haitambui hoteli ambayo imetajwa kukutana na viongozi wa halmashauri ili kuwapa fedha hizo.
“Nichukue nafasi hii kuwashauri kwamba suala hili limeshafahamika kama walikuwa na mpango huo basi fedha ambazo wanataka kuwahonga au kuwapatia wabunge wazitoe kwa NSSF wanaowadai, lakini kuwapa wabunge wa kamati hii ni kupoteza muda wao,” alisema Nkamia.
Kwa upande wake, Kabwe alieleza kusikitishwa na uvumi huo na kudai kuwa, maofisa wake walikuwa wakiwasiliana na uongozi wa kamati hiyo kutaka kujua ufafanuzi juu ya mambo ambayo wanapaswa kuwasilisha Dodoma.