Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma ili kukagua ujenzi wa uwanja huo unaofanywa na kampuni ya ujenzi ya Howard Humphrey
Katibu wa Halmashauri Kuu Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa Dk. Asha Rose Migiro , Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya na Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana wakielekea kwenye magari tayari kwa kukagua ujenzi wa uanjwa wa ndege wa Kigoma
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakikagua uwanja wa ndege wa Kigoma leo.
Mafundi wa kampuni ya Howard Humphrey wakiendelea na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma.
Meneja wa uwanja wa ndege wa Kigoma Injinia Clipia Tesha akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana wakati alipotembelea kukagua uwanja huo akiongozana na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya na kutoka kushoto ni Dk. Asha Rose Migiro Katibu wa Halmashauri kuu Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi CCM na Martin Shigela Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM.
Cleopa Mpembeni Meneja mradi wa Ujenzi wa Uwanja huo kutoka kampuni ya Howard Humphrey akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakati ujumbe huo ulipotembelea kukagua ujenzi wa uwanja huo leo
Meneja wa uwanja wa ndege wa Kigoma Injinia Clipia Tesha akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana kukagua ujenzi wa uwanja huo leo.