Afrika Kusini, wenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013, imefuzu kucheza hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya 2-2 na Morocco.
Kwa matokeo hayo Afrika Kusini inaongoza kundi A ikiwa na pointi 5 sawa na Cape Verde, lakini ikiizidi kwa wingi wa magoli.Katika mchezo wa leo Morocco ndiyo iliyoanza kufunga katika dakika ya kumi ya mchezo, likitiwa kimiani na El Adoua.
Matokeo hayo yaliyodumu hadi mapumziko.
Huku Morocco ikiamini kuwa imeshinda, ilishtukia Afrika Kusini wanasawazisha katika dakika ya 71 kupitia kwa Mahlangu.
Morocco haikukata tamaa kusaka ushindi, na iliwezakutia kimiani goli la pili katika dakika ya 82, mfungaji akiwa Abdelilah Elhafidi.
Afrika Kusini na Cape Verde ndizo zilizofuzu katika kundi A kucheza hatua ya robo fainali.
Morocco yenye pointi 3 na Angola yenye pointi 1 kutoka kundi A, zimeiaga michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2013.
Kundi B leo litakuwa linakamilisha michezo yake, kwa Ghana kumenyana na Niger, huku DR Congo ikipepetana na Mali.Mpaka sasa Ghana ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi 4, ikifuatiwa na Mali pointi 3, DR Congo pointi 2 na Niger imeweka kibindoni pointi 1.