TASWA FC YAFUNGWA 4-0 NA BAGAMOYO VETERANI

Kikosi cha timu ya Chama Cha waandishi wa habari za Mizhezo TASWA FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki kati yake na timu ya Bagamoyo Veteran uliofanyika kwenye uwanja wa Mawanakerenge Mjini Bagamoyo jioni ya leo, ambapo timu ya TASWA FC imechapwa magoli 4-0 na maveterani hao kutoka mjini Bagamoyo,Timu ya Waandishi wa habari ya TASWA FC imeshiriki katika mchezo huo ikiwa ni moja ya programu ya mkutano wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika kesho kwenye hoteli ya Kiromo View mjini Bagamoyo ambapo utafunguliwa na Ridhiwani Kikwete na Kufungwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ndugu Assah Mwambene.
Hiki ndiyo kikosi cha timu ya Bagamoyo Veteran kilichotoa kichapo kwa timu ya TASWA FC mjini Bagamoyo leo.
Baadhi ya waandishi wa habari ambao ni mashabiki wa timu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.




Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba Ibrahim Masoud katikati akizungumza na Mzee Willy Chiwango kutoka gazeti la This Day kulia na Beny Kisaka mkurugenzi mwanadamizi gazeti la Jambo Leo.
Mkuu wa Wilala ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wa pili kutoka kulia akizungumza na mwandishi mkongwe kutoka Zanzibar Said Salim huku wanahabari wengine wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mchezaji wa timu ya TASWA FC Juma Pinto akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Bagamoyo Veterani katika mchezo huo uliofanyika kwenyeuwanja wa Mwanakerenge mjini Bagamoyo
Mchezaji wa timu ya TASWA FC Shafii Dauda akimiliki mpirahuku beki wa timu ya Bagamoyo Veterani akiuwania katika mchezo huo, katikati ni mchezji wa timu ya TASWA FC Mohamed Akida.
Mshauri wa timu ya TASWA FC Masoud Sanani akihimiza wachezaji wa TASWA FC kucheza kwa bidii baada ya kuchapwa magoli 4-0 huku wachezaji wa timu hiyo wakishangaa wasijue la kufanya wakati zikiwa zimesalia dakika za majeruhi.
Previous Post Next Post