Shakira amejifungua mtoto wa kiume siku ya jana.
Mchumba wa mwanamuziki huyo ambaye ni mchezaji wa timu ya Barcelona Gerard Pique, ameandika katika mtandao wa Twitter kwa lugha ya kihispanyora akisema wamefurahi sana kupata mtoto wao wa kiume na wanashukuru sana kwa ujumbe wa watu mbalimbali waliowatakia Kheri.