Bilawal Bhutto Zardari, Mwanawe waziri mkuu wa Pakistan aliyeuawa, Benazir Bhutto, amezindua kuingia kwake kwenye siasa rasmi ikiwa ni maadhimisho ya miaka mitano tangu mamake kuuawa, Balawal ametangaza malengo yake kwa mara ya kwanza mbele ya maelfu ya wafuasi nyumbani mwao katika jimbo la Sindh.
Mamia ya maelfu ya wafuasi wa chama cha Pakistan Peoples Party walianza kufurika Larkana, kusubiri hotuba kuu kutoka kwa Bilawal Bhutto Zardari., wanaharakati waliobeba picha za Benazir Bhutto, na babake, waziri Mkuu wa zamani Zulfiqar Ali Bhutto, wamekita kambi kote mjini humo.
Bilawal aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho punde tuu baada ya kuuwawa kwa mamake na wapiganaji wa taliban mwaka wa 2007, lakini hajajitokeza hadharani kutokana na umri wake mdogo na kukosa uzoefu wa kisiasa.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 na aliyehitimu kutoka chuo cha Oxford, anaangaliwa kufufua umaarufu wa chama hicho, huku uchaguzi wa Bunge ukitarajiwa Pakistan mwaka wa 2013.
Tags:
News