TANZANIA MUSIC KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2012 KATIKA PICHA.

HAWA NDIO WATANGAZAJI WALIOTANGAZA KATIKA TUZO ZA KILI 2012


 
DIAMOND AKIWA NA QUEEN DARLING  


NI Balaa! Pamoja na majonzi yaliyotawala wakati shughuli inaanza kwa kumkumbuka marehemu Steven Charles Kanumba, Tuzo za Kili 2012 zilitawaliwa na mayowe ya kushangilia baadhi ya wanamuziki na bendi zenye upinzani mkali kufunikana kwa tuzo huku Naseeb Abdul ‘Diamond’ akitisha kwa mara nyingine, Ijumaa Wikienda lina fulu stori.
MLIMANI CITY PALIKUWA HAPATOSHI
Tukio hilo la kihistoria lilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar ambapo baadhi ya wasanii waliondoka kwa nyuso za furaha na wengine vilio kwa kukosa tuzo.
Shughuli ilianza saa mbili usiku kwa mastaa kusimama kwenye zulia jekundu kuonesha aliyevunja kabati huku kila mmoja akitaka kumnadi aliyemfanya kupendeza (madizaina).

KANUMBA AKUMBUKWA
Baada ya kumalizika zoezi la upigaji picha za kuuza sura, shughuli ilianza kwa kukaa kimya kwa dakika moja kumkumbuka marehemu Kanumba na baada ya hapo ilifuatia burudani ya nyimbo za asili kutoka kwa THT na wasanii wengine wa kizazi kipya.

ZOEZI LA UTOAJI TUZO LAANZA
Zoezi la utoaji tuzo lilianza bila mzuka lakini mambo yalivyosonga mbele ndivyo msisimko ulivyozidi kuongezeka.

MATOKEO
Katika kipengele cha Mtumbuizaji Bora wa Kike aliyeibuka kidedea ni Khadija Kopa huku Mtumbuizaji Bora wa Kiume akiwa ni Diamond.
Kwenye kinyang’anyiro cha Wimbo Bora wa R&B, Number One Fan wa Ben Pol ndiyo ulioibuka kidedea huku Wimbo Bora wa Hip Hop ukiwa ni Mathematics wa R.O.M.A.
R.O.M.A ndiye aliyeibuka Msanii Bora wa Hip Hop ambapo wimbo Bora wa Afrika Mashariki, tuzo ilikwenda kwa Jaguar wa Kenya kupitia wimbo wake wa Kigeugeu.
Katika kipengele cha Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka, tuzo ilikwenda kwa Maneck wa AM Records na Wimbo Bora wa Afro Pop, Hakunaga wa Suma Lee ulitisha.
Tuzo ya Msanii Bora Anayechipukia ilikwenda kwa Ommy Dimpoz ambapo Wimbo Bora wa Zouk Rhumba ulikuwa ni Dushelele wa Ali Kiba.
Katika kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana, tuzo ilikwenda kwa Ommy Dimpoz na Nainai aliomshirikisha Ali Kiba.
Katika Wimbo Bora wa Taarab, tuzo ilikwenda kwa Isha Mashauzi na wimbo wake wa Nani Kama Mama huku Twanga Pepeta ikiibuka na Wimbo Bora wa Kiswahili (Bendi) wa Dunia Daraja.
Aliyeibuka kidedea kwenye kipengele cha Rapa Bora wa Mwaka katika bendi ni Kalidjo Kitokololo huku Tuzo ya Video Bora ya Mwaka ikienda kwa Diamond.
Kwenye Wimbo Bora wa Mwaka, kama kawa tuzo ilikwenda kwa Suma Lee kupitia Hakunaga, ndipo Barnaba wa THT akafunga pazia kwa kuibuka Mwimbaji Bora wa Mwaka.

DIAMOND ATISHA TUZO ZA KILI 2012 
 Kwa matokeo hayo, Diamond aliendeleza rekodi yake ya mwaka juzi alipozoa tuzo tatu kwa mpigo huku akitoa zawadi ya tuzo moja kwa mama yake.





Previous Post Next Post