Shilole: Muziki dili kuliko movie,

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na muigizaji wa movie, Shilole au jina halisi Zuwena Mohamed amedai kuwa muziki ndio unaompa jeuri la kula bata mtaani.



Shilole aliyetamba na tracks kama Nakomaa na Jiji na Chuna Buzi, amesema kuwa muziki ndiyo unaomfanya aonekane mrembo na kutanua mtaani kwa kuwa unamwingizia fedha nyingi kuliko anazozipata katika movie.

Msanii huyo aliyedai kwa sasa yuko jikoni anaandaa ngoma ya kufunga mwaka itakayoingia sokoni mwezi ujao, alisema ameamua kuweka kando uigizaji kwa muda ili akusanye fedha kwenye muziki ili baadaye aweze kutengeneza movie yake.
Previous Post Next Post

Popular Items