Abdu Kiba amng’ang’ania Diamond

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdul Kiba, amepanga kutumia mbinu na ubunifu wa kila aina ili atoke zaidi na kuwafunika nyota mbalimbali nchini Tanzania.


Mwanamuziki huyo alisema miongoni mwa wanamuziki aliowakamia ni pamoja na Diamond ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akitamba na kutingisha katika majukwaa ya muziki.

Kiba ambaye ni ndugu wa staa mwingine wa muziki huo ambaye ni kaka yake, Ally Kiba ambaye ni mpinzani wa Diamond alisema anatarajia kufanya vizuri kupitia kazi zake kwani amejipanga kikamilifu kutangaza kipaji chake.
Previous Post Next Post