Uingereza kutuma majeshi kukabili Ebola

Uingereza inatuma wanajeshi 750 kwenda Sierra Leone kusaidia kupambana na mlipuko wa Ebola, alisema Waziri wa Ulinzi.

Wanajeshi hao watasaidia kujenga vituo vya matibabu katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.




BBC inaelewa Uingereza itatuma meli ya matibabu, RFA Argus na helikopta za Merlin.

Zaidi ya watu 3,400 wameshapoteza maisha wakati wa mlipuko wa Ebola, karibu wote wanatoka Afrika Magharibi. Nchini Sierra Leone vifo vinakaribia 678.

Save the Children imeripoti kiasi cha madhara kinachoendelea kuongezeka kwa kwa kasi nchini Sierra Leone, kukiwa na kesi tano kila baada ya saa.

Hakuna matibabu wala kinga ya Ebola, ambayo mpaka sasa imeshaathiri zaidi ya watu 7,200.
Previous Post Next Post