Huyu ndiye Mholanzi anayefukuzia ukocha katika timu ya Ghana

Gwiji Mholanzi Patrick Kluivert yuko kwenye orodha ya makocha watano wa Shirikisho la soka la Ghana ili kuwa kocha mpya.

Ghana imekuwa haina kocha tangu Kwesi Appiah aondoke mwezi Septemba.
Wagombea wengine ni kocha wa zamani wa Chelsea Avram grant, kiungo wa zamani wa Italia Marco Tardelli, Mswisi Michel Pont na Mhispania Juan Ignicio Jimenez.



“Pont, Kluivert na Tardelli watahojiwa mjini Accra Oktoba 17, Grant na Jimenez watahojiwa Oktoba 18, ilisema GFA.

Kluivert, ambaye alifunga magoli 40 kwa nchi yake katika mechi 79, aliacha kazi kama kocha msaidizi wa Uholanzi baada ya Kombe la Dunia.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona, 38, alianza kazi yake ya ukocha mwaka 2011 na kikosi cha Twente cha Uholanzi, ambapo alishughulika na vijana na timu za risevu.

Mwaka mmoja baadae alikuwa kocha msaidizi wa Louis van Gaal ambapo wawili hao waliipeleka Uholanzi hadi nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa