Sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Msami ila ukaribu wetu ulitokana na hii filamu 'Irene Uwoya'

Muigizaji wa filamu nchini Irene Uwoya amesema anajiandaa kuachia filamu yake mpya iitwayo ‘Kisoda’.  Uwoya amesema alisafiri hadi Afrika Kusini ili kutafuta location tofauti zitakazoifanya filamu hiyo kuvutia.


“Filamu ya Kigoda ni filamu ya aina yake katika filamu ambazo nimewahi kuzifanya,” alisema “Filamu inahusu drama and music, imeshagharimu pesa nyingi sana. Ndani utaona watu wakicheza muziki na maisha ya wasanii. Kwahiyo itakuwa tayari hivi karibuni na tutatangaza ikiwa tayar kwenda sokon.”

Katika hatua nyingine, Uwoya amekanusha uvumi kuwa ana uhusiano na msanii wa Soundtrack, Msami ambaye anadai ameshiriki kwenye filamu hiyo.

“Msami sijawai kuwa na mahusiano naye, alikuwa kama msanii mwenzangu. Hata ule ukaribu wake na mimi ambao ulizua tetesi za kuwa na mahusiano naye ni kutokana na hii filamu. Kwahiyo watu wajue ilikuwa ni kazi tu.”
Previous Post Next Post