Shilole ajiozesha kwa Mziwanda

Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa ‘Nakomaa na Jiji’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ au ‘Shishi Baby’ ameweka wazi kuwa mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki wa kizazi kipya, Nuh Mziwanda, ni zaidi ya mume kwake kutokana na jinsi anavyomjali.



Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Mziwanda kutuma picha mtandaoni akionyesha amechorwa tattoo nyingine yenye jina la mwanadada huyo.

Shilole alisema kwa jinsi anavyopendwa na kujaliwa na Mziwanda hana budi kumpa cheo cha mume hata kama bado hawajaoana.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa