Rapper Chidi Benz akamatwa na dawa za kulevya airport, alikuwa na shoo leo

Rashid Abdala Makwilo Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokiwa akieleke  jijini Mbeya kwenye show ya Instagram Party inayotarajiwa kufanyika leo.


Msanii Shetta ambaye alikuwa naye pamoja katika safari hiyo ya kuelekea Mbeya, amethibitisha kukamatwa na kwa Chidi akiwa na vitu vinavyohisiwa ni madawa ya kulevya.

“Kweli tulipata matatizo na Chidi pale airport ila mimi nikaruhusiwa yeye nikamuacha, amekamatwa na mambo mambo fulani sema ongea na wahusika watakwambia zaidi,” alisema Shetta.

Akizungumza na Millard Ayo, kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Selemani kamanda wa polisi katika uwanja wa ndege Dar es Salaam amesema Chidi Benz amekiri kuwa dawa hizo ni zake.

Amedai kuwa Chidi alikutwa na kete 14 za dawa za kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi iliyokuwa mifukoni mwake.

Chidi atapandishwa mahakamani hivi karibuni kwa kosa la kukutwa na dawa hizo.

Uthibitisho wa Chid Benz kukamatwa na dawa za kulevya...
Previous Post Next Post

Popular Items