Peter Okoye (P-Square) apata shavu la ubalozi wa Olympic Milk

Mmoja wa mapacha wa kundi la P-Square, Peter Okoye amechaguliwa kuwa balozi wa Olympic Milk.



Dili hilo linadaiwa kuwa la mamilioni ya naira. Hii ni mara ya kwanza kwa mmoja wa ndugu hao kusaini mkataba wake mwenyewe kwakuwa mikataba mingi husaini pamoja.

Wafuatiliaji wa burudani nchini Nigeria wanahisi hiyo inaweza kuwa ni dalili ya kutokuwepo maelewano mazuri kati yao. Kwenye tangazo la maziwa hayo, anaonekana Peter peke yake.
Previous Post Next Post