Nyota ya Diamond yazidi kung'aa ambwaga Davido kwenye tuzo za IRAWMA, awa Best African Entertainer

Diamond Platnumz amewabwaga Davido, Awilo Longomba, Willy Paul Msafi (Kenya) na Eddy Kenzo wa Uganda na kushinda kipengele cha ‘mtumbuizaji bora wa Afrika – Best African Entertainer kwenye tuzo za IRAWMA (International Reggae and World Music Awards).

“It always seems impossible until it’s Done!…ningependa kuwataarifu Wadau wangu kwamba #MdogoMdodo ndio nyimbo bora yenye Mahadhi ya Kiafrika na Kijana wenu Diamond ndio M’burudishaji bora wa Mwaka kwenye tunzo hizi za #IRAWMA zilizofanyika nchini Marekani 04|10|2014….. Asanteni sana sana…hakika Umoja ni nguvu, tuhamieni kwenye nyingine sasa,” ameandika msanii huyo kwenye Instagram.



Previous Post Next Post