Video: Navy Kenzo waeleza chanzo cha Weestar kutolewa kwenye kundi

Producer Nahreel na mpenzi wake Aika ambao wanaunda kundi la Navy Kenzo, wamesema sababu ya kinidhamu ndio ilipelekea kuondolewa kwa aliyekuwa member wa tatu wa kundi hilo, Weestar.

Nahreel ameuambia mtandao wa Bongo5 kuwa walimuonya mara kadhaa rapper huyo lakini mambo hayakubadilika.



“Kulikuwa na matatizo mengi kama discipline, vitu vingi vilikuwa vinatokea ambavyo vilikuwa vinaturudisha nyuma,” alisema.

“Tulimpa warning nyingi kwahiyo ikafika wakati tukasema ‘basi wewe labda ingekuwa vizuri ungesimama kama single artist sisi tukaendelea kama group,” aliongeza Nahreel.

Kwa upande mwingine, Nahreel amesema wanatarajia kuachia album iitwayo Niroge itakayokuwa na nyimbo saba au zaidi na wimbo wa kwanza ni ‘I Just Wanna Love You’ ambayo imetoka na video yake.



Previous Post Next Post