Mwimbaji wa Tmk aliyefariki Dunia YP, kuagwa TCC Chang’ombe na kuzikwa kesho (Oct 22) katika makaburi ya Chang’ombe

Msanii wa kundi la Wanaume Family YP aliyefariki usiku wa kuamkia leo kwa ugonjwa wa kifua, anatarajiwa kuagwa kesho (October 22) kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe na baada ya hapo atazikwa katika makaburi ya Chang’ombe karibu na maduka mawili.



Kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Family amesema mpaka sasa wapo kwenye maandalizi ya mazishi yatakayofanyika kesho saa kumi jioni.

“Kwa jinsi ratiba ilivyo msiba utakuwa nyumbani kwa baba yake, kwenye nyumba ya marehemu baba yake kwahiyo kesho tunatarajia tukiweza tumuage pale Chang’ombe na baada ya hapo tutazika kwenye makaburi ya Chang’ombe hapo karibu na maduka mawili,” amesema Saidi Fella.
Previous Post Next Post