Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu alidanganya umri, vielelezo vinamsuta, anaweza kuvuliwa taji muda wowote

Vielelezo zaidi ya vitatu vinaonesha kuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu alidanganya umri wake wa kuzaliwa.Vielelezo hivyo vinaonesha kuwa mrembo huyo ana umri wa miaka 25, na sio 23 kama cheti chake ambacho kinaaminika kughushiwa kisemavyo. Passport yake, leseni ya udereva na taarifa za website rasmi ya ‘Idara ya Usalama wa ndani ya Marekani (Department of Homeland Security), pamoja na profile yake kwenye mtandao wa exproletalent.com vinaonesha kuwa alizaliwa May 31, 1989 na sio May 31 1999


 Sitti alilazimika kupunguza miaka yake ili kwendana na sharti la mashindano ya Miss Tanzania yanayotaka mshiriki awe na miaka kuanzia 18 hadi 24. Hivyo kutokana na vielelezo hivyo, Sitti Mtemvu ana asilimia 100 za kuvuliwa taji na kupewa mshindi wa pili.



Leseni ya udereva ya Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu
Kama uamuzi ambao kwa sasa upo mikononi mwa Baraza la Sanaa la Taifa, BASASA na wizara husika utakuwa vingine, huo utakuwa mwanzo wa kushuka kwa uhalali wa mashindano hayo pamoja na sifa za mamlaka hizo. Dalili za kuwepo udanganyifu huo, zilizoongezeka zaidi pale Mtemvu alipokutana na waandishi wa habari ambapo pamoja na kuwashutumu kwa kuandika habari za uongo, maelezo yake yalikuwa na walakini.

Taarifa za Sitti Mtemvu kwenye exproletalent.com zinaonesha kuwa ana umri wa miaka 25

Cheti cha kuzaliwa alichonacho sasa kinaonesha kuwa kilitolewa September 9 mwaka huu.

Sitti alitumia pia fursa hiyo kukanusha tetesi kuwa ana mtoto. “Sina mtoto, na mkitaka tunaweza kwenda hospitali sababu naona kama mmekuwa mkiniandama kwa vitu ambavyo si vya kweli,” alisema.
Akijibu swali la kuonekana kwa passport yake inayoonesha kuwa alizaliwa mwaka 1989 na huku kwenye cheti alichoonesha kikionesha amezaliwa May 31, 1991, Sitti alisema:

Sitogusia hilo suala kwasababu mimi nilivyokuwa nakuja kuomba ‘Umiss Tanzania’ niliombwa cheti cha kuzaliwa sasa hivyo vitu vingine ni personal life, kwahiyo sidhani hata nyie kama kuna mtu atakuja anachukua passport yetu, ama driving licence ya kweli au feki na kuiweka kwenye mtandao kama ni kitu ambacho mngependelea.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited Hashim Lundenga alisema kuwa nafasi ipo wazi kwa wale wenye mashaka na umri na maisha ya Sitti kupeleka vielelezo halisi ambavyo watavifanyia kazi.

“Tukishapata proof tutazifanyia kazi vizuri sana na mwenye haki atapata. Sisi hatuwezi kumvua taji, vitahusika BASATA na wizara husika,” alisema Lundenga.

BASATA imepewa siku saba kufuatilia ukweli juu ya umri wa Sitti Mtemvu, na kwa vielelezo hivyo visivyojificha, hakuna shaka litakuja na uamuzi sahihi, kumvua taji hilo.

Credit:Bongo5
Previous Post Next Post