Majuto anautaka ubunge wa CCM

Msanii mkongwe wa maigizo nchini Tanzania, King Majuto amesisitiza kuwa dhamira yake ya kugoombea ubunge si masihara na kueleza kuwa atafanya kwa vitendo anayoyasema.

Majuto aliieleza Taarifa News jana kuwa hatanii na na kwamba atawania ubunge kupitia kwa tikieti ya Chama cha Mapinduzi—CCM.


Alisema lengo ni kuwainua wasanii ambao kwa muda mrefu wamekuwa hawana msaada kwa serikali.

King Majuto aliyeanza kazi tangu miaka ya 80, ni mmoka wa waigizaji wenye kipaji cha kuchekesha watu kwa kiasi kikubwa.

Licha ya uhodari alionao, kwa kiasi kikubwa ameanza kunufaika na kipaji chake akiwa uzeeni. Kazi za ujanani zilikuwa hazilipi zaidi ya kusifiwa kila alikokuwa akipita.

Je akiwa pale Dodoma unadhani atasaidia wasanii wenzake kuwa maslahi bora zaidi? Ni endapo atashinda kura za maoni na hatimaye kupata idhini ya kuingia bungeni.
Previous Post Next Post

Popular Items