Hii hapa ni Thamani ya Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ni mwanamichezo bora kuwahi kutokea na ana thamani ya euro bilioni 1, kwa mujibu wa wakala wake, Jorge Mendes.




Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli 19 kwenye michezo yote 11 katika mashindano yote msimu huu na kuna uwezekano mkubwa wa kushinda tuzo ya Ballon d’Or tena. Mendes – anayedai kuwa Ronaldo ataondoka Madrid akiwa na miaka 40, licha ya tetesi kupewa ofa na Manchester United, anaamini kuwa mteja wake ni mwanamichezo bora zaidi kuwahi kutokea duniani.

“Ni mchezaji bora kwenye mchezo mkubwa duniani wenye ushindani kuliko mingine. Kwa sababu hiyo, ni mwanamichezo bora duniani,” alisema.

Wakala huyo alipoulizwa ni gharama gani ambayo club inayomtaka inatakiwa, Mendes alijibu; “The price that is stated in his release clause – €1bn.”
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa