Viwango vya FIFA: Tanzania yapanda na kufikia hapa

Mabingwa wa Kombe la Dunia, Ujerumani wameendelea kuwa juu ya msimamo wa timu bora za taifa duniani kwa mujibu wa orodha iliyotangazwa na Shirikisho la Soka la Duniani – FIFA.



Matokeo hayo hayashangazi sana hasa kutokana na viwango vya timu zilizoshikilia nafasi 10 bora wakiwemo pia Argentina, Colombia na Ubelgiji – zote zilifanya vizuri katika World Cup kule Brazil na pia katika michuano ya hivi karibuni.

Waliokuwa mabingwa wa dunia Hispania wameshuka sana mpaka nafasi ya 10.

Kwa hapa nyumbani Afrika Mashariki, Tanzania imepanda juu nafasi tano kutoka ya 115 mpaka ya 110.



Tanzania imekuwa nje ya top 100 kwa miaka kadhaa, je kasi hii mpya ni ya muda mfupi?

Kenya imeporomoka mpaka nafasi ya 116 wakati Uganda ni ya 84 .Lakini Congo DR imejikakamua na katika nafasi ya 60 duniani.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa