Diamond atoa sababu za kuchelewa kwa ndoa yake na Wema Sepetu

Mapenzi ya Wema na Diamaond yamedumu kwa muda mrefu licha ya mikwaruzano ya hapa na pale laikin wawili hao wameweza kudumu katika mapenzi kwa muda  na Kama mambo yangeenda yalivyokuwa yamepangwa, baada ya Ramadhan, Wema Sepetu angekuwa akiitwa Wema Naseeb! Lakini kutokana na sababu mbalimbali Diamond Platnumz alisogeza mbele mipango ya kufunga ndoa na mpenzi wake huyo.


“Kabla ya Ramadhan ilikuwa tufunge ndoa kabisa, lakini mambo yakaingiliana,” Diamond alikiambia kipindi cha The Sporah Show. “Mtoto naye ni majaliwa sio kama sitaki, hajanipangia bado. Nataka sana sana lakini siwezi sema sana kwa sababu unajua kuzaa pia ni makubaliano na wewe na mpenzi wako. Labda pia mwenyezi Mungu hajataka haujafika wakati muafaka. Kuna vitu fulani tunaviweka sawa ili tuwe safe zaidi na hata tukizaa isiwe wazazi wangu au wazazi wake wakajisikia vibaya,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Diamond alisema hajamtenga baba yake kama inavyoandikwa kwenye magazeti ya udaku.

“Mzee Abdul sina matatizo naye baba yangu, bahati mbaya sikubahatika kukaa naye sana,” alisema Diamond. “Sometimes naendaga kwao sio mara kwa mara. Unajua vingi vya uongo na wanaandika vingi, sema sikubahatika kukaa na baba yangu sana ndio maana sikuweza kujua yeye na mama yangu wana matatizo gani”

So nilivyokua nikaona mzee wangu hakunisaidia mpaka nakua ni kimpango wangu. Nimetoka lakini nikaona haiwezi kusaidia kitu nilivyokuwa nakaa sometimes ninaweza nikaenda, lakini haiwezi kuwa sawa na mama yangu. Watu wanajaribu kutengeneza kwasababu wananiona nipo karibu sana na mama, wakiona niko karibu na mama na wakipima ukaribu wangu na baba unaonekana ukaribu wa mama ni mkubwa sana,” alisisitiza.

“Sasa inakuwa ni ngumu kwa sababu nimeshamzoea mama yangu. Sema kwa sasa nina muda sana sijaonana naye kiukweli na muda mrefu sijaenda na nini. Lakini kila siku nikikaa na mama yangu ananiambia ‘msamehe yule ni baba yako’ Sometimes anadhani mimi bado nina kinyongo. Mama yangu ni mtu ambaye ananisihi sana ananiambia ‘nenda kwa baba yako usifanye hivyo kama vitu vilitokea na vimeshapita’,’ Nimeshamsemehe.”


Previous Post Next Post