AliKiba amkana Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba amekana mashairi ya kutumia wimbo wake wa ‘Mwana Dar es Salaam’ kumuimba msanii mwenzake Nassib Abdul ‘Diamond’.

Wimbo huo kwa sasa umekuwa ukitambaa kwenye mitandao ya kijamii huku kila mstari wa nyimbo hiyo ukitafsiriwa kama fumbo kwa Diamond.



Mwanamuziki huyo alisema ujumbe uliyopo katika wimbo huo ni somo kwa jamii nzima ya kitanzania, kwani yale yote aliyozungumzia yamekuwa yakitokea.

Hakuna shaka kuwa huo ni mwendelezo wa tofauti za wasanii hao ambao katika siku za hivi karibuni wameripotiwa kutokuwa na maelewano mazuri baina yao kwa sababu ambazo hazijawa wazi.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa