Picha za harusi ya Angelina Jolie na Brad Pitt zillizouzwa kwa shilingi bilioni 3.3

Mastaa Angelina Jolie na Brad Pitt.ambao kwa pamoja hujulikana kama Brangelina wameuza picha zao za harusi kwa dola milioni 2, ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 3.3 za Tanzania. Kiasi hicho cha fedha kimepatikana baada ya kulipwa na majarida mawili ya People na Hello!, wiki moja baada ya kufunga ndoa Aug. 23 nchini Ufaransa.



Hiyo sio mara ya kwanza Pitt, 50, na Jolie, 39, wameingiza fedha kutokana na maisha yao binafsi licha ya kuwa na maisha ya usiri. Wawili hao wala hawana msemaji wao.

Mwaka 2006, waliuza picha za kwanza za mtoto wao wa kike, Shiloh kwa jarida la People kwa dola milioni 4.



Mwaka 2007, Jolie na Pitt walifanya kazi na People na Hello!, tena kwa kuuza picha za kwanza za mtoto wao wa kiume, Pax kwa kiasi ambacho hakikujulikana.

Mwaka 2008, walidaiwa kulipwa dola milioni 14 na jarida la People kuchapisha picha za kwanza za watoto wao mapacha, Vivienne Marcheline na Knox Leon. Kwa pamoja wawili hao wana utajiri wa dola milioni 385.

Previous Post Next Post