Picha: Wasanii na Serengeti watoa msaada wa milioni 3 kwa hospitali ya mkoa wa Mara

Wasanii wa muziki wakishirikiana na kampuni ya bia ya Serengeti leo wametoa msaada wa shilingi milioni tatu kwa hospitali ya Mkoa wa Mara kwaajili ya kununulia madawa na vifaa vingine vitakavyosaidia matibabu ya majeruhi wa ajali ya mabasi iliyotokea Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 35.





















Shilole akikabidhi misaada hiyo

Akizungumza katika hospitali hiyo, rapper Stamina ambaye aliwawakilisha wasanii, alisema wametoa kidogo walichonacho ili kusaidia huduma katika hospitali hiyo. “Japo sio kikubwa lakini tunadhani kitaisadia kwa mamna moja,” alisema Stamina.

Kwa upande wa mwakilishi wa bia ya Serengeti, alisema wameamua kuungana na wasanii kwa pamoja ili kutoa msaada wao kwa hospitali hiyo.




Previous Post Next Post

Popular Items