Picha: Hii ndio familia ya Rapper ya Inspector Haroun, Ndoa yake yatimiza miaka 10, hii ndio siri ya kudumu kwake

Unaweza kumuita 'Babu' mkali wa Rap Cartoon , Inspector Haroun ametimiza miaka 10 katika Ndoa yake. Rapper huyo wa ‘Mtoto wa Getu Kali’ alifunga ndoa na mke wake May 5 mwaka 2004.

Mke wa Inspector akiwa na wanae, Shadya na Nassir



Mwaka 2004 ndoa ya Inspector ilipofungwa

Tulifanya sherehe ndogo ya kifamilia lakini ndani ya mwezi wa kumi mwaka huu tunataka kufanya sherehe kubwa ya kuadhimisha miaka kumi ya ndoa yetu sababu nataka nisherehekee na fans wangu pamoja na mashibiki wote wa muziki kwa ujumla,” Inspector ameiambia Bongo5. “Nitawaambia rasmi itakuwa wapi, lini na tarehe gani. Nashukuru Mungu kunifikisha hapa na familia yangu pia kutujalia afya njema.”



Mrs and Mrs Haroun Kahena

Wanandoa hao kwa sasa wana watoto wawili, Nassir na Shadya.

“Siri ya mafanikio yetu kila mmoja kukuubali udhaifu wa mwenzie na kujikinga na skendo pia kudhamiria kuishi ndani ya ndoa na kuhimili misukosuko ya kila aina haijalishi hata nikiyumba kwa kipato huwa tunavumilia na kuchukua kama changamoto za maisha yetu,” amesema Babu.

Mke wa Inspector akiwa na wanae, Shadya na Nassir

 Nassir

 Shadya

Watoto wa Inspector, Shadya na Nassir



Watoto wa Inspector, Shadya na Nassir
Previous Post Next Post