Jaji anayeendesha kesi ya Oscar Pistorius ametupilia mbali hukumu ya kuua kwa kukusudia (premeditated murder), kwa kusema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kuwa mwanariadha huyo alimuua mpenzi wake kwa makusudi baada ya majibizano.
Jaji Thokozile Masipa amedai kuwa aliridhishwa kuwa mtuhumiwa alikuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya baya na zuri. Hata hivyo amesema kuwa hiyo haina maana kuwa hana hatia.
Kutokana na uamuzi huo wa jaji, mwanariadha huyo atakuwa na muda mfupi kiasi wa kutumikia kifungo jela.
Utetezi wa Pistorius ni kuwa hakutekeleza mauaji hayo kwa makusudi bali alidhani kuwa mpenzi wake alikuwa ni mwizi aliyetaka kumvamia.

Tags:
celebrity News