Nick Cannon akanausha tetesi za yeye kugombana na Mariah Carey

Mchekeshaji Nick Cannon amekanusha taarifa zilizotolewa wiki kadhaa zilizopita kuwa yeye na mkewe Mariah Carey wana ugomvi mkubwa na kwamba hawaishi nyumba moja kwa zaidi ya miezi mitatu.

Nick Cannon ameonesha kuwa maelezo hayo yalitengenezwa na hayakutolewa kwake na kwamba yeye asingeweza kusema hivyo.



“Trouble in Paradise” is the dumbest phrase I’ve ever heard! I would never say that s***” Ametweet kwa hasira katika moja ya tweet yake.
Unaweza kujiuliza alikuwa wapi muda wote huo kukanusha, lakini kwa kufahamu swali hili Nick Cannon amelitolea majibu.

“Binafsi nimekuwa nje ya mitandao ya kijamii miezi kadhaa iliyopita kwa sababu za kawaida lakini najisikia hitaji la kutaka kuzungumzia.”

Nick amemsifu sana Mariah kwenye tweets zake akimuita mama bora aliyembariki kwa kumpatia watoto.
Previous Post Next Post