‘Umebadilika’ itakuwa video yangu bora kuliko video zangu zote nlizowahi kufanya "Young Killer"

Rapper Young Killer Msodoki, amedai kuwa video ya wimbo wake ‘Umebadilika’ aliomshirikisha Banana Zorro itakuwa bora zaidi kuliko video zote alizowahi kufanya.



Video hiyo iliyoongozwa na Hefemi Studios imefanyika katika visiwa vya Mbudya jijini Dar es Salaam.

Msodoki ameiambia Kikwetu Blog kuwa uzuri wa video hiyo utachangiwa na mandhari aliyoyatumia ambayo yatapendezeshwa na muonekano wa bahari na fukwe za Mbudya, watu watakaoonekana na picha ujuzi wa Hefemi anayesifika kwa video zake zenye ubora wa hali ya juu.

Rapper huyo mshindi wa tuzo za KTMA 2014 kwenye kipengele cha msanii bora, anayechipukia amesema video hiyo inatarajia kutoka wiki mbili kuanzia sasa.
Previous Post Next Post