Mengi, Ngowi na Shanker waing'arisha Tanzania kwenye All Africa Business Leaders Awards

Wafanyabiashara watatu wa Tanzania wameshinda kwenye tuzo za ‘All Africa Business Leaders Awards’, AABLA zilizoandaliwa na CNBC Africa na kutangazwa Nairobi, Kenya September 20.



Patrick Ngowi, Jacqueline Ntuyabaliwe na Reginald Mengi

Hizo ni tuzo za biashara Africa zinazoheshimiwa zaidi zilizoandaliwa kuwatambua watu waliofanya mambo makubwa kwenye biashara zao. Tuzo za East African Business Leader of the Year and Lifetime Achievement Award zote zimeenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dr Reginald Mengi.

Mwenyekiti Mtendaji na mwanzilishi wa kampuni ya Technobrain Limited ya Tanzania, Manoj Shanker alinyakua tuzo ya Entrepreneur of the Year. Nayo tuzo ya East Africa’s Young Business Leader of the Year imechukuliwa na mwenyekiti mtendaji wa Helvetic Solar, Patrick Ngowi.


Patrick Ngowi akiwa na tuzo yake
Previous Post Next Post