Kuna baadhi ya wasanii wakubwa wa bongo ambao hulipisha wasanii wadogo wanaowaomba kufanya nao collabo, lakini kwa Nay Wa Mitego mambo yako tofauti.
Nay ambaye ameachia video mpya ya ‘Mr Nay’ hivi karibuni, amesema yeye huwa halipishi msanii kwa sababu naye aliwahi kufanyiwa hivyo akiwa anataka kutoka.
“Mimi kiukweli kabisa hela nilizonazo zinanitosha, ninazopata zinanitosha still naendelea kutafuta, mi simtozi msanii malipo ya featuring hasa kwa undergrounds, mi simtozi kabisa kwasababu mimi nimetokea huko, kuna watu walishawahi kunikaziaga wakisemaga nilipe kiasi flani…kuna wengine walishasema nilipe laki 3 halafu kipindi hicho laki 3 unarekodi studio ukilipa unarekodi karibu nyimbo mbili au tatu.
Niliona sio fair nilisononeka sana nilisema namwomba mwenyezi Mungu siku moja na mimi nije kuwa mkubwa ili niwasaidie hawa ambao wanahitaji kupiga step kwenda mbele ndio maana mimi simlipizi mtu, hakuna msanii yeyote ambaye nilishawahi kumwambia nilipe kiasi flani, huwa napenda nikiona ngoma nzuri basi ntaenda kufanya kwa moyo mmoja.” Alisema Nay kupitia 255 ya XXL.
Collabo ambazo Nay ameshirikishwa hivi karibuni ni pamoja na ‘Simu Ya Mwisho’ ya Kala Jeremiah, pamoja na ‘Kwenu Vipi’ ya Stamina inayofanya vizuri kwa sasa hasa wanapoi perform kwenye show za Fiesta.