Mwanadada Lady Jay Dee amefunguka leo kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii kuwa Kuna uwezekano mashabiki wa Lady Jaydee wakaachwa ‘yatima’ kwa muda usiojulikana bila kupikiwa chakula kipya (wimbo) baada ya Jide kuweka wazi kuwa yupo kwenye kipindi ambacho hana hisia za kuandika nyimbo mpya.
Lakini hata hivyo Jide ameongeza kuwa lolote linaweza kutokea muda wowote na kubadilisha hali hiyo na kuamua kutoa wimbo mwingine baada ya ‘Nasimama’ wakati wowote kwasababu ‘hatabiriki’.
Kupitia ukurasa wake wa facebook hiki ndicho alichokiandika Lady Jaydee:
“Hiki ni kipindi ambacho siwezi kutunga/kuandika nyimbo, sina hisia zozote na nikilazimisha hazitakuwa nzuri”
“Huwa nakaa hata miaka 3 au 5 pengine mwezi mmoja au miwili au 6 , yaani huwa haitabiriki, pale inapotokea tu ndio huwa.
Natumaini jibu hili ni muafaka na litawaridhisha walio uliza, Poleni kwa kusubiri, i wish ningeweza”.
Je unadhani huenda ni kutokana na matatizo yake ya ndoa?